Formula ya Kuandaa dawa ya Asili ya Mafua - 1Kg

 


UGONJWA: MAFUA AU MATATIZO YA UPUMUAJI

CHANZO: BAKTERIA/ VIRUSI AU MAZINGIRA MABAYA YA BANDA/NYUMBA YA KUKU(NDEGE)

VIUNGO, MIMEA NA MITISHAMBA KWA AJILI YA TIBA NA KINGA

(KILLO 1)

 

 N0.

KIUNGO/MMEA/MTI

KIASI (GRAMU)

KIASI (VIJIKO VYA CHAKULA)

1.

Mdalasini

400

40

2.

Manjano

100

10

3

Pilipili Manga

200

20

4

Tangawizi

100

10

5

Kitunguu Thoum

100

10

6

Oregano

60

6

7

Mrehani/Basil

40

4

 

JUMLA  (UJAZ0)

1000

100

NOTE:-

Kwenye mchanganyiko huu, kuna vuingo/mimea au miti kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili ili kupigana na vimelea vya magonjwa, kuna viungo vya kuongeza hamu ya kula na kunywa, vitamin na kuuchangamsha mwili.

 

MATUMIZI (DOSAGE)

A.      KAMA KINGA

Kuku wapewe Mchanganyiko wenye mimea/miti/viungo hivyo uliochanganyika vizuri kwenye maji ya kunywa kwa kipimo cha gramu 5 (Kijiko cha chai) kwenye maji lita 3 mara 3 kwa wiki au gramu 10 (Kijiko cha Chakula) kwenye Kilo moja ya chakula chao. Kwa Matokeo bora zaidi nivyema kuwapa kwenye maji na kwenye chakula.

 

B.      KAMA TIBA.

Kuku wapewe Mchanganyiko wenye mimea/miti/viungo hivyo uliochanganyika vizuri kwenye maji ya kunywa kwa kipimo cha gramu 10 (Kijiko cha chakula) kwenye maji lita 4 kwa siku 3-5 mfululizo kwa wiki au gramu 20 (Vijiko viwili vya Chakula) kwenye Kilo moja ya chakula chao. Kwa Matokeo ya haraka zaidi nivyema kuwapa kwenye maji na kwenye chakula.

 

UANDAAJI

Ni vyema Mchanganyiko wa kwenye maji kuandaliwa na kupewa ukiwa umejichanganya na maji angalau Dakika 30 au Saa 1 ili viungo/Mimea ikolee vizuri kwenye maji. Mchanganyiko wa lwenye maji unaweza kutumika ndani ya masaa 48 (Siku 2) bila kuharibika.

Mchanganyiko Uliolala kwenye maji unakuwa Umekolea vizuri zaidi.

Inaweza kutumiwa na vifaranga kuanzia siku ya 3 tokea kutotolewa.

No comments:

Powered by Blogger.