Utambuzi wa Magonjwa ya Kuku Kupitia Kinyesi
Kupitia Table hii, tunaweza kujifunza jinsi ya kutambua magonjwa mbalimbali ya kuku na ndege wafugwao kwa kuangalia kinyesi chao.
pia kuona aina ya dawa stahili.
S/NO |
AINA YA UGONJWA |
RANGI/MWONEKANO WA KINYESI |
DALILI NYINGINE |
1 |
MDONDO(Newcastle) |
kuku hujisaidia kinyesi cha kijani |
Kupinda shingo, kurudi kinyuma nyuma,
kutokwa na ute mzito mdomoni |
2 |
TYPHOID (Homa ya Matumbo) |
Kuku hujisaidia Kinyesi cheupe ambacho |
Kuvimba baadhi ya Viungo |
3 |
GUMBORO
(IBD) |
Vifaranga Hujisaidia kinyesi cha majimaji
cheupe. |
Vifaranga Hutoa Mlio wa Kulia kila anapokuwa anajisaidia. |
4 |
COCCIDIOSIS
(Kuhara Damu) |
Awali kuku hujisaidia Kinyesi cha Ogoro na baadae huharisha damu
iliyochanganyika |
Kujikunyata/Kuvaa Koti na Manyoya
Kutimka.(Rough) |
5 |
FOWL CHORELA (Kipindupindu) |
Kuku hujisaidia Kinyesi cha Njano |
Kuku hukonda sana, na kuwa mwepesi mno. |
6 |
POLLORUM |
Vifaranga Hujisaidia kinyesi cheupe na
hugandiwa na kinyesi sehemu za Haja. ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga
kabla ya wiki nne |
Vifaranga Kujikunyata na Kudumaa kwenye
ukuaji. |
7 |
MINYOO |
Kinyesi chenye mchanganyiko wa rangi na Brown
kwa mbali. |
Minyoo huonekana kwenye kinyesi na
Kupiga miayo sana kwa kuku wakubwa. |
8 |
MAFUA |
Kinyesi huwa cha kawaida |
Kupiga chafya, Kukoroma, kupumulia
mdomo. Macho Kujaa maji au utandu mweupe na
kuziba. |
9 |
NDUI |
Kinyesi huwa cha kawaida |
Vidonda au vipele kwenye uso, puani na
baadhi mdomoni na machoni hadi kwenye upanga. |
10 |
UKOSEFU WA VITAMIN/LISHE DUNI |
Kinyesi huwa cha kawaida |
Shingo Kupinda, Miguu kupinda, Macho
kutoa machozi na utando mweupe hadi kuziba. |
No comments: