Utangulizi
Ukiacha changamoto ya Gharama kubwa za Chakula kwenye ufugaji, Gharama nyingine huwa ni za madawa, ya kinga na Tiba. Kama mfugaji, yakupasa kuwakinga kinga kuku/ndege wako dhidi ya Magonjwa yote, yawe ya Virusi , Bacteria, Protozoa n.k.
Magonjwa ya Virusi hukingwa kwa kutolewa chanjo, miongoni mwa magonjwa hayo ni:-
1. Mareks/Mahepe
2. Newcastle/Kideri/Mdondo
3. IBD/ Gumboro
4. Fowl Pox/ Ndui
Ki kawaida kuku/ndege wasiopata chanjo dhidi ya magonjwa hayo juu, hufa sana na hakua Tiba ya Kihospitali zaidi ya Kuwapa Vitamins na Antibiotics ili kuimarisha Kinga zao za mwili na kuwapa hamu ya kula maana katika hali ya ugonjwa, kuku/ndege hupunguza au kuacha kula kabisa.
Magonjwa ya Bacteria na Protozoa baadhi hutolewa kinga na mengine hutibika pindi yanapojitokeza mfano:-
1. Magonjwa ya matumbo na kuhara kama Coccidiosis, Typhoid ,Cholera n.k.
2. Magonjwa ya mfumo wa hewa na upumuaji kama Mafua
3. Minyoo.
Magonjwa yanayosababishwa na Lishe Duni na Uhaba wa Viirutubisho mfano:-
1. Kuvimba macho(Mabuja) – Upungufu wa Vitamin A
2. Matege, Kupinda Miguu au Kushindwa Kutembea – Upungufu wa Calcium (DCP)
3. Kupinda Shingo, Kuweweseka (Crazy & Wary Chick) na Kuificha Shingo - Upungufu wa Vitamin E
Kwa wafugaji wengi wa zama hizi kumekuwa na changamoto sana ya Magonjwa ya matumbo kwa kuku wazazi ambayo hupelekea kupata watoto wagonjwa, jambo ambalo hupelekea Ukuaji duni na vifo vingi sana vya vifaranga.
Kuna baadhi ya viumbe Mungu huwajaalia kuzaliwa na kinga ya asili juu ya baadhi ya magonjwa na huwa hawauugui yaweza pita hata miaka kadhaa (Resistant/Immune), lakini pia wengine huipata ama kuiboreshaa kinga yao ya kawaida na kuipeleka kwenye ngazi za kuwa Immune/Resistant kwa baadhi ya magonjwa.
Katika mazingira yetu ipo baadhi ya mimea ambayo miti, majani, magome,mizizi au maua yake husaidia kwa kiasi kikubwa kutibu maradhi mbalimbali na pia kupandisha kiwango cha kinga za mwili.
Kupitia Tafiti mbalimbali, wanazuoni wengi wamekiri Mimea/Viungo kama Kitunguu Thoum, Aloevera, Pilipili, Majani ya Mpapai, Majani ya Muarobaini, Majani ya Mpera, Majani ya Muembe, Majani ya Mstafeli na Majani ya Oregano kwa kuyataja machache hutibu maradhi mbali mbali na kupandisha Kinga za mwili kwa viumbe wengi ikiwemo Binadamu na ndege kama Kuku.
Kwa Heshima kubwa Naomba Niitambulishe kwenu, Immune Booster , Huu ni mchanganyiko uliopimwa na kujaribiwa (Measured & Tested) wa viungo na mimea yenye uwezo wa kutibu na kupandisha kinga za mwili za ndege wetu wafugwao kwa kiasi cha kuwafanya kuwa Immune/Resistant kwa Baadhi ya magonjwa mengi.
Kwa Dose sahihi, Immune Booster haina madhara kwa ndege na huweza kutumiwa pamoja na dawa zingine za hospitali ikiwa Utapenda kufanya hivyo au ukiwapa yenyewe tu.
Sisi, Kuku Care Tanzania Tunapenda Kuwashauri wafugaji wenzetu kuendelea kutumia na kufuata kanuni za ufugaji bora ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu zote za chanjo dhidi ya maradhi yoote ya virusi kuanzia siku ya kwanza ya kutotolewa kwa kifaranga.
Pia kwa wale wafugaji wanaoishi kwenye mazingira yenye changamoto za upatikanaji wa dawa/chanjo za Hospitali basi ni vyema kwao kuendelea kutumia Tiba Mbadala kwa kiwango sahihi kama kingi, tiba na Ulinzi dhidi ya Magonjwa.
No comments: