LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu.
Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu
300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku
sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka
mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo
(Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa
kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo
wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa
hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula
mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili
ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya
Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike
pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya
miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa
shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza
banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi
ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku
wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km
papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana
futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi,
Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2
n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au
nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka.
Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1
ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni
Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea
(incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga
200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni
wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha
kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya
kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi
huu utakuwa unajiendesha wenyewe.
Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240
kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa
hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya
mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja
na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na
Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha
aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula
chochote.
No comments: