GHARAMA ZA MADAWA ZINAVYOUMIZA WAFUGAJI KUKU



Habari za Leo ndugu zangu wafugaji.
Naomba tuchukue muda kutathmini Ni namna gani gharama za dawa za kuku/Ndege zinavyotuumiza wafugaji na kutafuna sehemu kubwa ya mapato au mitaji yetu.
Kinachopelekea Gharama hizi kuwa kubwa na kuongezeka kila Mara Ni :-
*1. Usugu wa Magonjwa*
Baadhi ya magonjwa yamekuwa sugu mabandan na kuwa na Tabia ya kujirudia kila mara kwa Mara na kumfanya mfugaji amalize Nguvu nyingi kwenye madawa.
*2. Matumizi hasi ya Dose.*
Kuna baadhi ya wauzaji maduka ya dawa hutoa dose si sahihi kwa mfugaji, hii hupelekea ugonjwa kupoozwa na kutoisha Mabandani kwetu.
*3. Dawa za Kuchakuchua*
Baadhi ya madawa yamechakachuliwa hivyo kusababisha kushindwa kufikia lengo.
Pia utunzaji Mbaya baada ya kufungua kwa ajili ya matumizi nayo huathir Nguvu ya dawa, mfano kuwekwa juani au kukaa wazi.
*4. Mazingira Dhaifu ya Mabandani*
Wafugaji wengi wamekazana kutibu tatizo Bila kukumbuka kuondoa *chanzo Cha tatizo*.
Unaweza poteza gharama nyingi kutibu mafua kumbe mzunguko wa hewa bandani kwako si Safi na salama.
Unaweza Tibu Coccidiosis typhoid na Cholera mpaka Basi kumbe vyombo vina backteria, maji yako si salama na wakati mwingine dodoki lako la kuoshea drinkers limejaa bakteria tupu.
*USHAURI WANGU*
1. Wafugaji wenzangu, tujihidi kujua sababu za Magonjwa ili kupunguza matumizi makubwa ya madawa na kupelekea usugu wa Magonjwa na kutupunguzia Faida.
2. Tutenge Muda kupiga hesabu ya gharama za madawa kwa Mwezi au kwa Batch ili kujipanga na njia mbadala.
3. Tujiunge Kama wanafamilia wa Bidhaa za Organic ili tusaidiane kupata Tiba na Lishe Mbadala za Mifugo yetu kwa Nusu Gharama za kawaida huku tuki maximize Faida zetu.
*Kwa Pamoja, tutapunguza vifo, gharama za chakula, Magonjwa na kuboresha Faida zetu*
Hussein,
Kuku Care
*0784 645 900 au 0788 654 574*

No comments:

Powered by Blogger.