UTARATIBU MZURI WA KUTUMIA BIDHAA ZA KUKU CARE(DOSAGE)
Habari za Leo ndugu mfugaji?
Ufuatao ni utaratibu mwepesi ambao una matokeo Mazuri zaidi katika kuwapa Herbs/Bidhaa za KUKU CARE Ndege wako.
IKIWA WANAUMWA:-
1. Chukua mchanganyiko wa Herb husika Mfano; Mafua Herbs/Stomach Herbs au Multi Boosters Herbs VIJIKO VITATU (3) Weka kwenye maji lita 2.5 koroga vizuri kwenye chombo chake, kisha chukua chakula cha Kuku au Ndege wako pima Kilo 7. Baada ya hapo changanya Maji yaliyokolea dawa (2.5 Lita) na hizo kilo 7 za chakula kiwe mash au pellet usijali.
Hakikisha hata kama una kuku wengi angalau wapate mara moja/awamu moja kwa siku chakula chenye mchanganyiko huu au vyema zaidi wakila hivi *Siku 3 Mfululizo bila kuwapa chakula kisicho changanywa na mchanganyiko huu ili wapone haraka.
2. Chota vijiko 6 au gram 60 za Herbs wape kwenye Maji ya kunywa Lita 20. Ni vyema kuanza kuweka herbs kwanza kasha kujaza maji kwenye ndoo ili mchanganyiko uwe umekolea na kujichanganya vizuri.
KWA MATOKEO YA HARAKA NI VYEMA KUWAPA KWENYE MAJI NA CHAKULA MFULULIZO BILA KUACHIA KATI IKIWA WANAUMWA.
IKIWA HAWANA DALILI ZA KUUMWA:-
1. Chukua mchanganyiko wa Herb husika Mfano; Mafua Herbs/Stomach Herbs au Multi Boosters Herbs VIJIKO VITATU (3) Weka kwenye maji lita 3 koroga vizuri kwenye chombo chake, kisha chukua chakula cha Kuku au Ndege wako pima Kilo 8. Baada ya hapo changanya Maji yaliyokolea dawa (3 Lita) na hizo kilo 8 za chakula kiwe mash au pellet usijali.
Hakikisha hata kama una kuku wengi angalau wapate mara moja/awamu moja kwa siku chakula chenye mchanganyiko huu au vyema zaidi wakila hivi Siku 3 Mfululizo bila kuwapa chakula kisicho changanywa na mchanganyiko huu ili Waboreshe kinga zao na Kuponesha Magonjwa ambayo hayajaanza kuonesha Dalili.
2. Chota vijiko 3 au gram 30 za Herbs wape kwenye Maji ya kunywa Lita 20. Ni vyema kuanza kuweka herbs kwanza kasha kujaza maji kwenye ndoo ili mchanganyiko uwe umekolea na kujichanganya vizuri.
KWA MATOKEO YA HARAKA NI VYEMA KUWAPA KWENYE MAJI NA CHAKULA MFULULIZO BILA KUACHIA KATI KWA WASTANI WA SIKU 3-4 KWA WIKI.
Kuku Care Tz
0784 645 900 au 0788 654 574.
Tandika Magorofani, Temeke, DSM.
No comments: