Formula ya Tiba Asili ya Homa ya Matumbo (Fowl Typhoid)
UGONJWA: HOMA YA MATUMBO (FOWL TYPHOID)
CHANZO: BAKTERIA NA ULAJI WA VYAKULA VYA ASILI YA BAHARINI AMBAVYO HAVIPIKWA
VIUNGO, MIMEA NA
MITISHAMBA KWA AJILI YA TIBA NA KINGA
(KILLO 1)
N0. |
KIUNGO/MMEA/MTI |
KIASI (GRAMU) |
KIASI (VIJIKO VYA CHAKULA) |
1. |
Muarobaini |
250 |
25 |
2. |
Unga wa Majani ya Mpapai |
200 |
20 |
3 |
Mrehani/Basil |
150 |
15 |
4 |
Oregano |
150 |
15 |
5 |
Manjano |
90 |
9 |
6 |
Aloevera |
70 |
7 |
7 |
Mdalasini |
90 |
9 |
|
JUMLA (UJAZ0) |
1000 |
100 |
NOTE:-
Kwenye mchanganyiko huu, kuna vuingo/mimea au miti kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili ili kupigana na vimelea vya magonjwa, kuna viungo vya kuongeza hamu ya kula na kunywa, vitamin na kuuchangamsha mwili.
MATUMIZI (DOSAGE)
A. KAMA KINGA
Kuku wapewe Mchanganyiko wenye mimea/miti/viungo hivyo uliochanganyika vizuri kwenye maji ya kunywa kwa kipimo cha gramu 5 (Kijiko cha chai) kwenye maji lita 3 mara 3 kwa wiki au gramu 10 (Kijiko cha Chakula) kwenye Kilo moja ya chakula chao. Kwa Matokeo bora zaidi nivyema kuwapa kwenye maji na kwenye chakula.
A. KAMA TIBA.
Kuku wapewe Mchanganyiko wenye mimea/miti/viungo hivyo uliochanganyika vizuri kwenye maji ya kunywa kwa kipimo cha gramu 10 (Kijiko cha chakula) kwenye maji lita 4 kwa siku 5-7 mfululizo kwa wiki au gramu 20 (Vijiko viwili vya Chakula) kwenye Kilo moja ya chakula chao. Kwa Matokeo ya haraka zaidi nivyema kuwapa kwenye maji na kwenye chakula.
UANDAAJI
Ni vyema Mchanganyiko wa kwenye maji kuandaliwa na kupewa ukiwa umejichanganya na maji angalau Dakika 30 au Saa 1 ili viungo/Mimea ikolee vizuri kwenye maji. Mchanganyiko wa lwenye maji unaweza kutumika ndani ya masaa 48 (Siku 2) bila kuharibika.
Mchanganyiko Uliolala kwenye maji unakuwa Umekolea vizuri zaidi.
No comments: