JIFUNZE VITU AMBAVYO HUTAKIWI KURUHUSU KUKU 🐓 WAKO ALE.

 


Kuna baadhi ya vitu uwa tunawapa kuku kwa mazoea au tunawaachia tu tunapoona wanakula lakini ukweli vinakuwa na madhara ebu tuviangalie;
*VITUNGUU*
vitunguu vina sumu iitwayo thiosulphate ambayo huua seli hai nyekundu. Iwapo utalisha kwa kiwango kikubwa itasababisha upungufu wa damu(anaemia) au kifo.
*MAHARAGWE MABICHI AU YASIYOPIKWA.*
Maharagwe mabichi au yasiyopikwa yana sumu iitwayo hemaglutin ambayo ni hatari kwa kuku kwahiyo unashauriwa kupika au kuchemsha kuondoa sumu hii.
*MCHELE MKAVU.*
Kuku wanaolishwa Mchele mkavu kuna hatari mchele huo kujikusanya tumboni na kusababisha matatizo.
*MAGANDA YA PARACHICHI🥑*
Kuku wanapokula maganda ya parachichi itapelekea kuingiza sumu mwilini kwahiyo epuka maganda ya parachichi yasije kujichanganya na chakula.
*MBEGU ZA APPLE🍎*
Mbegu za apple zina sumu iitwayo cynade japokuwa kuku wanapenda apples hakikisha unatoa mbegu.
*VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI.🍚*
Vyakula vyenye chumvi nyingi husababisha ugonjwa uitwao hypernatremia kwahiyo mwili wa kuku hauitaji kiasi kikubwa cha chumvi. Kuku wanaweza kuvumilia kiasi kidogo cha chumvi nacho ni 0.25% kwenye maji. Endapo kutakuwa na uhaba inaweza kupelekea ugonjwa huo.
Credit:-*Keystone Kuku Farm 🇹🇿

No comments:

Powered by Blogger.